WhatsApp Image 2023-11-06 at 11.58.47

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya afungua kongamano la Miaka 3 ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi

Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Novemba 5,2023 alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la kuadhimisha miaka mitatu (3) ya Uongozi wa Rais WA Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi

Kongamano hilo limetayarishwa na Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango pamoja na taasisi zake ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu mbali mbali walialikwa katika kongamano hilo, miongoni mwa Vyuo Vikuu vilivyoshiriki ni pamoja na Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA), Chuo Cha Utawala WA Umma(IPA), Chuo Cha Mwalimu Nyerere, Zanzibar University (ZU) pamoja na Al Sumeit Cha Chukwani

Lengo la kongamano hilo ni kuyaelezea Mafanikio ya Miaka mitatu (3) ya Dkt Mwinyi Madarakani

Katika Kongamano hilo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil aliwasilisha Ripoti ya utekelezaji ya Miaka mitatu ya Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na kueleza kuwa Miaka mitatu Dkt Mwinyi Miradi mbalimbali ya Maendeleo imetekelezwa, Miradi ya Skuli, Hospitali, Barbara, Bandari na kuongeza pencheni jamii kutoka 20,000/ Hadi 50,000/ pamoja na nyongeza ya mishahara

Aidha, taasisi za ofisi ya Rais Fedha na Mipango zilipata fursa za kuwasilisha taarifa zao za utekelezaji wa Miaka mitatu, taasisi zilizowasilisha taarifa zao ni Shirika la Bima la Zanzibar, Benkj ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Mamlaka ya Manunuzi pamoja na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA)

Nao, baadhi ya wanafunzi walipata fursa ya kuelezea Mafanikio ya Dkt. Mwinyi, Ali Ahmada kutoka Chuo Kikuu Cha Summeit Chukwani ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kwa kazi kubwa wanayoifanya kuleta Maendeleo na kuiomba Serikali kuongeza kiwago Cha Fedha za mikopo Kwa wanafunzi WA vyuo vikuu

Aisha Mussa kutoka Chuo Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) ameitaka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango kuwapatia elimu na mafunzo wajasiriamali juu ya matumizi ya Mifumo ya kidigitali katika kazi zao

Imetolewa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mioango.

Tags: No tags

Comments are closed.