Lengo Kuu

LENGO KUU la Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ni kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali, usimamizi wa matumizi wa fedha za Umma, Usimamizi wa deni la Taifa pamoja na kutoa huduma za Uhasibu Serikalini.

MAJUKUMU YA MSINGI YA OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO

 

 • Kusimamia mapato ya Serikali kutokana na vyanzo mbali mbali, mapato hayo yanajumuisha mapato ya ndani na kodi na yasiyokuwa ya kodi.
 • Kusimamia mali za Serikali kupitia usimamizi wa ununuzi, utunzaji na
  uondoshaji wa mali za serikali pamoja na Hisa za serikali katika Mashirika
  ya umma.
 • Kusimamia Fedha za Umma na Shughuli za Uhasibu Serikalini
 • Kusimamia Deni la Taifa.
 • Kusimamia Maendeleo ya Sekta ya Fedha inayohusisha masuala ya Benki,
  Bima, Hifadhi ya Jamii, Soko la Hisa na Mitaji.
 • Kusimamia Teknolojia ya habari na Mawasiliano kuhusiana na mapato,
  matumizi na Malipo ya Serikali