Idara hii inasimamiwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali, akisaidiwa na Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali. Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali ndiyo inayosimamia masuala ya kiuhasibu na fedha katika Serikali ikifuata muongozo wa Sheria ya Fedha namba 12 ya mwaka 2016.
Majukumu ya Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali
- Kuandaa uwasilishaji wa matarajio ya mapato na matumizi kwa Kamati ya Ukomo ya Serikali (Government Ceiling Committee).
- Kuandaa usuluhishi wa Kibenki kwa Hesabu zote za Hazina ya Serikali (Forex and Local Accounts).
- Kutayarisha taarifa zinazoonesha vifungu tofauti vya budget, Fedha iliyotengwa, hesabu na usimamizi wa kihasibu wa kila siku.
- Kudhibiti matumizi kwa kulinganisha na mapato na kuhakikisha uwepo wa ukwasi (Liquidity Position).
- Kuanzisha na kuweka daftari linaloonesha faida/hasara za Amana za Serikali.
- Kuhakikisha kuwa Mfumo wa Matumizi ya Serikali unafanya kazi kwa ufanisi na udhibiti mzuri na unawawezesha watumiaji wote wa mfumo katika kufanya kazi zao za kila siku na kuweza kutatua kasoro zinazojitokeza katika utendeaji.
- Kusaidia uandaji wa taarifa za kifedha kwa watumiaji na kuhakikisha kuwa taarifa zote ziko sahihi.
- Kusaidia ufungaji wa Hesabu za mwaka, kufanya usimamizi wa usanidi “configuaratuion” wa mfumo kwa kasma mpya na kuhamisha taarifa za bajeti kwenye mfumo.
- Kuwasimamia watumiaji wa mfumo kapata haki za utumiaji, kuweka usalama mzuri kulingana na sera na taratibu za usalama na kufanya mapitio ya utaratibu uliopo na kusaidia kupata taarifa zilizopita, za ndani na nje kwa kuzingatia uhalisia.
- Kusimamia ufunguzi na uendeshaji wa Hesabu za Serikali na kufuatilia bakaa la hesabu hizo.
- Kufuatilia na kuratibu Bodi ya Uchunguzi wa Fedha taslim na Stamp na kutoa mapendekezo.
- Kushirikiana na Kamati za Uchunguzi wa Hesabu za Serikali na Kamati ya Fedha za Baraza la Wawakilishi zinazohusiana na maswala yaliyopo na yanayojitokeza katika Kamati.
- Kuongoza, kuratibu na kutekeleza shughuli zote za mageuzi ya usimamizi wa Fedha za Umma katika Taasisi za Umma.
- Kusajili, kutathmini na kusimamia kampuni binafsi za kihasibu na kodi.
- Kutathmini ufuataji wa Sheria ya Fedha, Kanuni na viwango vya usimamizi wa kihasibu vya kimataifa na washauri wa kodi kwa huduma wanazotoa.
- Kutayarisha makisio ya riba ya Deni la Umma na malipo ya Kima kwa ajili ya kuiingiza katika bajeti ya mwanzo.
- Kutimiza matakwa ya Serikali kifedha na kuweka gharama ndogo na madeni kadiri iwezekavo zinazohusiana na vihatarishi.
- Kutunza kumbukumbu za Madeni ya Serikali na kufuatilia mfumo wa Usimamizi wa madeni.
- Kutoa dhamana na kuweka kumbukumbu za malipo ya dharura kwa Taasisi za Umma, mashirika na Serikali za mitaa.
- Kutoa taarifa za mwenendo wa Fedha katika Mfuko Mkuu, malipo ya deni na salio la mtawanyo wa mkopo.
- Kutoa kazi za sekriterieti ya Kamati ya Usimamizi wa Deni la Zanzibar
- Kuandaa na kutoa taarifa mbali mbali, kupokea muhtasari wa mishahara kwa kasma zote kwa ajili ya kutayarisha mshahara na madai ya mshahara ya mwezi kwa kasma za serikali na kuziwasilisha “Exchaquer” kwa mlipaji Mkuu kwa taratibu zinazofuata.
- Kusahihisha na kuhifadhi nyaraka tofauti zilizotumika katika taratibu za malipo na kuweka kumbukumbu za wafanyakazi wote walioidhinishwa na kasma zao kuchukua nyaraka za malipo.
- Kuhakikisha usimamizi mzuri wa matumizi ukilinganisha na zile huduma ambazo kisheria zinalipwa moja kwa moja kutoka katika Mfuko Mkuu.
- Kusimamia Kituo cha Pamoja cha Malipo ambacho matumizi yote kutoka kwa watoa huduma wanalipwa kwa niaba ya Serikali.
Idara hii inaundwa na Divisheni Kuu sita (6) ambazo ni: –
a) Divisheni ya Usimamizi wa Fedha.
b) Divisheni ya Usimamizi wa IFMS.
c) Divisheni ya Uhasibu na Utawala.
d) Divisheni ya Fedha na Deni la Taifa
e) Divisheni ya Usimamizi wa Matumizi