Divisheni ya usimamizi wa matumizi unashughulika na usimamizi wa malipo ya Serikali.

Majukumu ya Divisheni ya Usimamizi wa Matumizi

  • Kufanya malipo kwa kasma zote kupitia hesabu za Serikali za Amana, Maendeleo, Matumizi ya kawaida na Deni la Taifa, ambazo zinajumuisha kurikodi majalada, kutengeneza, kuwasilisha kwa idhini, kuidhinisha, mchakato wa malipo, kurikodi na kuwasilisha majalada ya Fedha kwa njia ya mtandao “EFT” na kutoa orodha ya hundi ya kila na kupeleka Benki Kuu na kupokea Taarifa ya kibenki ya kila siku kwa ajili kufanya suluhidhi la Hesabu.
  • Kupokea na kukusanya malipo, taarifa mbali mbali za malipo kama vile orodha ya hati ya malipo, hundi iliyopitiwa na muda kutoka katika kasma zote kwa jili ya kutoa hundi, uthibitisho wa malipo, taarifa baada ya malipo na kutoa orodha ya hundi kutoka katika mfumo wa malipo na kuweka kumbukumbu za miamala ya kila siku.
  • Kufanya usajili wa watoa huduma katika Mfumo wa Malipo na kusimamia malipo kwa kurudisha Fedha katika kifungu husika cha bajeti kwa kasma husika kwa kushirikiana na “Core Application Team” na kukamilisha “Debit Memo”.
  • Kuandaa na kutoa taarifa mbali mbali, kupokea muhtasari wa mishahara kwa kasma zote kwa ajili ya kutayarisha mshahara na madai ya mshahara ya mwezi kwa kasma za serikali na kuziwasilisha “Exchaquer” kwa mlipaji Mkuu kwa taratibu zinazofuata.
  • Kusahihisha na kuhifadhi nyaraka tofauti zilizotumika katika taratibu za malipo na kuweka kumbukumbu za wafanyakazi wote walioidhinishwa na kasma zao kuchukua nyaraka za malipo.
  • Kuhakikisha usimamizi mzuri wa matumizi ukilinganisha na zile huduma ambazo kisheria zinalipwa moja kwa moja kutoka katika Mfuko Mkuu.
  • Kusimamia Kituo cha Pamoja cha Malipo ambacho matumizi yote kutoka kwa watoa huduma wanalipwa kwa niaba ya Serikali.