Kitengo hiki kinahusika nakutoa huduma za ununuzi na na usimamizi wa uondoshaji wa mali za umma ndani ya Ofisi. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo.

Majukumu ya Kitengo cha Ununuzi na Uondoaji wa Mali za Umma

  • Kusimamia kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za umma katika Taasisi ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali ya Umma isipokuwa maamuzi na utoaji wa mikataba;
  • Kusaidia kazi za Bodi ya Zabuni;
  • Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni;
  • Kutoa huduma za Sekretariati ya Bodi ya Manunuzi ya Ofisi ya Rais Fedha na Mipango. 
  • Kupanga Mpango wa Ununuzi na Mpango wa Uondoshaji wa Mali za Umma ya Ofisi;
  • Kupendekeza taratibu za ununuzi na uondoshaji wa mali za umma;
  • Kutayarisha na kupitia vigezo vitakavyotumika kwenye Zabuni;
  • Kutayarisha nyaraka za zabuni;
  • Kutayarisha matangazo ya Zabuni;
  • Kutayarisha nyaraka za mikataba na kutoa nyaraka za mikataba zilizothibitishwa;
  • Kuziweka na kuzihifadhi taarifa na taratibu zilizotumika katika ununuzi na uondoshaji wa mali za umma;
  • Kuunganisha shughuli za ununuzi na uondoshaji wa mali za umma kwa Idara zote.
  • Kununua, kutunza na kusimamia usambazaji wa malighafi, vifaa na huduma mbalimbali za Ofisi; 
  • Kuandaa, kutunza na kuhuisha daftari la mali mbalimbali za Ofisi;
  • Kuandaa orodha ya vifaa katika kila ofisi.