Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya ushauri na udhibiti wa mali na fedha za Ofisi, Kufanya ukaguzi wa matumizi ya rasilimali za Ofisi. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango
Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
- Kutoa ushauri bora kuhusiana na matumizi ya rasilimali za Ofisi;
- Kufanya Ukaguzi wa matumizi na mapato kwa kazi za kawaida na maendeleo (Miradi ya Ofisi);
- Kutoa ripoti ya awali (first draft) na ripoti ya mwisho (Final Report) ya Ukaguzi kwa Taasisi/Idara iliyokaguiwa kwa wakati;
- Kuratibu Vikao vya Kamati ya Ukaguzi ‘Audit Committee’;
- Kufanya ukaguzi wa matumizi ya rasilimali za Ofisi na kuandaa taarifa; Kufanya ukaguzi wa taratibu na mifumo ya utendaji kazi;
- Kufanya ufuatiliaji wa maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
- Kuandaa taarifa na kufanya ukaguzi kwa mujibu wa thamani ya fedha (Value for money).