WhatsApp Image 2024-01-23 at 08.54.33_51d33f48

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum ameendesha kikao cha Jukwaa la Uchumi na Bajeti kwa upande wa Serikali kuu kwa mujibu wa sheria ya Fedha.

Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amewataka wanasheria wote wa serikali na makatibu wakuu kuacha kusaini mkataba wowote wenye vipengele vya kodi na baadae kuomba kusamehewa kodi kwani hiyo sio kazi yao kwani msamaha wa kodi unatolewa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango na msamaha unautaratibu wake ambao upo kisheria .

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza hayo wakati akifungua Jukwaa la bajeti la mwaka 2024/2025 kwa serikali kuu liloshirikisha makatibu wakuu katika ukumbi wa Shekh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni.

“Tufahamu kuwa kodi inayokusanya ndio sisi inayotulipa mishahara, huduma za afya, elimu na huduma nyengine za barabara, maji, pencheni zinatokana na hii kodi,” alisema.

Hivyo, aliahidi kwamba Ofisi yake itaendelea kulisimamia jambo hilo ili kuona kunakuwa na nidhamu ya ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuangalia namna bora ya kuhakikisha kila mmoja anawajibika katika usimamizi wa sheria za kodi nchini.

“Jambo hili tutaendelea kulisisitiza ili kufikia utekelezaji wa bajeti kwa zaidi ya asilimia 100 na jambo hili linawezekana ikiwa kila mmoja wetu atakuwa mlinzi wa kodi ambazo ni fedha za umma,” alisisitiza.

Waziri Saada akizungumzia bajeti zinazotaarishwa kuzingatia masuala ya kijinsia alisema bado kuna muamko mdogo kuhusiana na utayarishaji wa bajeti unaozingatia jinsia hasa kunufaika kwa wanawake katika masuala mbalimbali ikiwemo kilimo, afya na mambo mengine.

Alisema pamoja na kujaribu kujenga uwezo kwa watendaji lakini jambo hilo bado halijafanikiwa hivyo Ofisi yake itahakikisha inaweka nguvu kubwa katika baadhi ya wizara tano ikiwemo Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Elimu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini na Wizara ya Uchumi wa Bluu ili kuona namna gani wataweza kutekeleza bajeti zinazozingatia jinsia.

Mbali na hayo Waziri Saada alisema wizara italifanyia kazi eneo la manunuzi na eneo la mapato ili kuhakikisha manunuzi yote yanayofanywa serikalini yanazingatia sheria.

“Mara hii tunakwenda kwenye bajeti ambayo ya uhalisia utaingiziwa fedha na kazi zako utaonesha unazotakiwa uzifanye kisingizio cha kuwa huna pesa hujafanya hicho kitakuwa kimeisha.

Jukwa hilo limehudhuriwa na Viongozi wakuu wa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango.

Aidha, washiriki wa jukwaa hilo walimuomba Mwenyekiti kuzingatia mijadala yao
Sambamba na hayo walisisitiza kuomba kuwa miradi ya kimkakati kusimamiwa na serikali kuu na sio Idara au Mashirika ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati.

Jukwaa hilo lipo kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa fedha za umma ambapo mada mbalimbali za uchumi na matumizi ziliwasilishwa na kuzingatia matumizi na makusanyo ya bajeti kwa mwaka 2024/2025.

Tags: No tags

Comments are closed.