WhatsApp Image 2023-11-06 at 11.51.51 (1)

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya azindua Bodi ya ZIAAT

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Novemba 3,2023 amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi (ZIAAT) katika Ukumbi wa taasisi hiyo uliopo katika jengo la iliyokuwa Ofisi ya Mfuko wa Barabara Maisara Mjini Zanzibar

Mhe. Waziri amewataka wajumbe wa Bodi hiyo wawe wabunifu na wasimamie taasisi Kwa maslahi ya Umma pamoja na kufanya uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Dkt. Saada ameshauri kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa (ZIAAT) wapitie vizuri Sheria ya (ZIAAT) na wafanye maboresho ya kuingiza masuala ya miamala ya fedha katika Sheria za kiislam pamoja na mambo mengine

Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi Bw. Juma Amour Mohammed ameeleza kuwa Bodi itafanya kazi Kwa uweledi wa hali ya juu katika kuboresha tasnia ya uhasibu na Ukaguzi pamoja na kutoa elimu Kwa wajumbe wa Bodi ili wafahamu Sheria ya (ZIAAT)

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi CPA. Ame Burhan Shazil ameeleza kuwa taasisi hii imeanzishwa Kwa Sheria No 7 ya Mwaka 2022 malengo yake ni pamoja na kuongeza ubora wa huduma zitolewazo na (ZIAAT), kuwatambua na kuwasajili Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa kodi

Katika hafla hiyo, pia alikuwepo Muwakilishi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi CPA Charles Masabu ambae ameitaka (ZIAAT) kufanya kazi zake kitaalamu zaidi na wakianza tu kuwasajili Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi ni vyema wakasajiliwa Kwa njjia ya kieletroniki na hili litarahisisha ukusanyaji wa Kodi

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha n Mipango

Tags: No tags

Comments are closed.