Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

wizara ya Fedha na Mipango

Uncategorized

Uncategorized

ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA SERIKALI

WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Juma Malik Akil, ameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Kwa Fedha za Serekali.  Amesema miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za Serikali ni lazima kuzingatia mipango kazi, malipo na muda uliowekwa wa kukamilika. Dk. Akil alisema hayo wakati akizungumza baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo Mji wa Serikali Kisakasaka, AFCON City, Bandari ya Fumba na Bandari ya Mangapwani, ili kujionea hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo. Alisema ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo ni muhimu katika kuhakikisha fedha zinazotengwa na Serikali zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na utekelezaji wake ukifanyika kwa kuzingatia viwango, mpango kazi na muda uliowekwa. Aidha alisema  ziara hiyo imelenga  kuhakikisha fedha zinazotengwa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na matokeo yake yanaonekana kwa wananchi. Akizungumzia mradi wa Mji wa Serikali Kisakasaka, alisema unatarajiwa kuwa na majengo ya Wizara mbalimbali za Serikali hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa nafasi za ofisi zinazozikabili taasisi za serikali. Alisema mradi huo, ambao umeanza kutekelezwa katika kipindi cha miezi sita hadi minane iliyopita, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24, huku utekelezaji wake ukiwa umefikia takribani asilimia nane. Kwa upande wa AFCON City ya Zanzibar, alisema mradi huo umefikia asilimia 85 ya utekelezaji, kutokana na kuanza kutekelezwa mapema ukilinganisha na baadhi ya miradi mengine. Alibainisha kuwa  mbali na uwanja mkuu, mradi huo unahusisha viwanja vya mazoezi, eneo la kuogelea na jeti itakayowezesha vyombo mbalimbali vya usafiri wa majini kuwafikisha abiria wanaotarajiwa kufika Zanzibar kwa ajili ya michezo.  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar,  Akif Ali Khamis, alisema Bandari ya Fumba inatarajiwa kukamilisha ujenzi wa gati yake Januari 2027 na kuanza rasmi kutoa huduma Februari mwaka huo, ikiwa na uwezo wa kupokea meli kubwa zenye urefu wa zaidi ya mita 350 na kina cha mita 14.5. Alisema utekelezaji wa ujenzi wa ghati hiyo umefikia takribani asilimia 80, huku mradi mzima ukiwa umefikia asilimia 60, na awamu ya kwanza ya bandari hiyo ikitarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia takribani makontena 300,000. Alisema uwezo huo utaifanya bandari hiyo  kuwa na nafasi kubwa katika kupunguza msongamano wa mizigo katika Bandari ya Malindi.

Uncategorized

HAFLA YA MAKABIDHIANO YA MAGARI YA USAFI

Wizara ya Fedha na Mipango imekabidhi kwa Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Malumu za SMZ gari za usafi 26 ikiwemo Tipper 15 na Compactor 11 Kwa ajili ya ukusanyaji wa taka ngumu katika Manispaa za Unguja na Pemba. Hafla ya Makabidhiano hayo ilifanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango tarehe 8 September 2026 katika Ukumbi wa Tume ya Mipango na kushuhudiwa na watendaji wa Wizara zote mbili. Ununuzi wa magari haya ulifanyika kupitia taratibu za ununuzi za Mradi wa BIG-Z kwa kuzingatia masharti na taratibu husika za manunuzi za Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Magari haya ni mapya na yanatumia teknolojia ya kisasa ambayo yatasaidia katika usimamizi na udhibiti wa matumizi yake. Kwa mfano: Magari ya Compactor yatafungwa GPS na kamera maalumu kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa matumizi yake na kuimarisha ufanisi wa madereva watakaotumia magari hayo. Akizungumza katika Makabidhiano ya gari hizo, mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil amesema hana shaka kuwa magari hayo yatatumika kama yalivyokusudiwa kutokana na imani kubwa ya Utendaji na Usimamizi kwa Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali  za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ. Kiujumla gari hizo zimewekewa lengo la ukusanyaji na usafirishaji wa taka, kuboresha usafi wa mazingira katika maeneo yanayohudumiwa na Manispaa, usafirishaji wa vifaa na taka kwenda maeneo maalumu ya utupaji, kusaidia shughuli za usimamizi wa jaa kuu la Kibele na maeneo mengine yanayohusika, kupunguza changamoto ya uhaba wa vitendea kazi katika Serikali za Mitaa na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi wa Unguja na Pemba. Dkt. Juma Malik Akil amesema Serikali inalengo la kuweka miji katika hali ya usafi na haiba ya kuvuti Kwa kununua gari maalum za ukusanyaji wa taka ngumu kupitia mradi huu.  Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Aboud Hassan Mwinyi amesema jumla ya Bilioni 7 TSh, ndizo zimetumika katika ununuzi wa gari hizo ambazo zimetengenezwa kutoka kiwandani kama toleo la mwaka 2026 chini ya usambazaji wa kampuni za GF Trucks and Equipment Limited ya Dar es Salaam na Kampuni ya GANSU CONSTRUCTION INVESTMENT HEAVY INDUSTRY TECHNOLOGY CO.LTD ya CHINA Nae Mhe. Idrisa Kitwana Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali  za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ ameishukuru  Wizara ya Fedha na Mipango Kwa kukabidhi gari hizo kwani kumekuwa na mahitaji  makubwa ya magari ya ukusanyaji taka katika manispaa   zote za Unguja na Pemba. Wakati huohuo Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Tamisemi  ilisaini hati ya  makubaliano ya gari hizo.

Uncategorized

MKUTANO WA KUJADILI UTEKELEZAJI WA ZADEP II

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil, amezitaka sekta binafsi nchini kushirikiana kwa karibu na Serikali katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar wa Miaka Mitano wa Awamu ya Pili (ZADEP II), ili kufanikisha malengo ya maendeleo na kukuza uchumi jumuishi. Dk. Akil alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa ZADEP II  uliowakutanisha viongozi wa Serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo, huko Golden Tulip Uwanja ndege Zanzibar. Alisema  ushiriki wa sekta binafsi unapaswa kwenda zaidi ya kuhudhuria mikutano pekee bali ni  kuwa sehemu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo, ambapo  Serikali pekee haiwezi kufikia malengo ya maendeleo bila ushiriki madhubuti wa sekta hizo. Kwa upande wake, Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa na Maendeleo ya Kisekta kutoka Tume ya Mipango Zanzibar Mohemed Masoud Salim alisema Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 inalenga kuifikisha Zanzibar katika hadhi ya uchumi wa kipato cha kati cha juu ifikapo mwaka 2050 kupitia maendeleo endelevu na jumuishi. Alieleza kuwa Dira ya Zanzibar 2050 imejengwa katika nguzo nne kuu ambazo ni mageuzi ya kiuchumi, maendeleo ya rasilimali watu na huduma za kijamii, miundombinu na uunganishaji pamoja na utawala na ustahimilivu. Mapema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Josephine Rogate  Kimario alisema mkutano huo umelenga kuwakutanisha Serikali na sekta binafsi ili kujadili namna ya kufadhili na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar wa Miaka Mitano wa Awamu ya Pili .

Uncategorized

WIZARA YASAINI MKATABA WA UJENZI KATIKA MRADI WA KUIMARISHA MAENEO YA UTALII KATIKA VIJIJI VYA CHWAKA NA MAKUNDUCHI

Wizara ya Fedha na Mipango imefanikiwa kusaini mkataba wa ujenzi kupitia Mradi wa BIG-Z unaohusu kuimarisha maeneo ya utalii katika vijiji vya Chwaka na Makunduchi. Mradi wa kuimarisha maeneo ya Utalii unaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ambao ndio wadau wakuu wanaosimamia mradi huu. Hafla ya utiaji saini wa mkataba huo imefanyika tarehe 11 Agosti, 2026, ambapo mkataba huo umesainiwa rasmi na Kaimu Katibu Mkuu Ndugu Aboud H. Mwinyi na Ndugu Suhaila Salum Mbarak ambae ni Katibu kutoka kampuni ya SECCO (SMC-Private) Limited. Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Aboud Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora wa kazi za ujenzi, usimamizi mzuri wa muda pamoja na uratibu madhubuti wa utekelezaji wa miradi hiyo. Aidha, alimtaka mkandarasi kufanya kazi kwa uweledi ili kukamilisha mradi huu kwa wakati uliopangwa kwa mujibu wa Mkataba na kwa gharama iliyopangwa. Pia mkandarasi huyo alitakiwa kuhakikisha kuwa na mpango kazi ulioandaliwa vizuri ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo hauleti usumbufu kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayotekelezwa miradi hiyo. Kwa upande wa mkandarasi ameahidi kuyafanyia kazi yale yote ambayo yameanishwa katika mkataba pamoja na kuyapokea yaliyoelezwa na Mhe. Aboud. Pia ametoa shukrani kwa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuiamini kampuni yao kwa kuwapa kazi kubwa kama hii hasa kwa kuwa Utalii ni suala muhimu sana katika Visiwa vya Zanzibar. Mradi wa Kuimarisha Maeneo ya Utalii Katika Vijiji vya Chwaka na Makunduchi unadhamiria kuboresha  nyuumba za kihistoria za Sultan Rest House na British Rest House, maeneo ya bustani na soko la Samaki katika Kijiji cha Chwaka pamoja na kuimarisha maeneo ya wazi likiwemo eneo la Kiutamaduni la Sherehe za Mwaka Kongwa lililopo katika Kijiji cha Makunduchi.

Uncategorized

Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Maafisa Ununuzi Zanzibar, 2026

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akil, amewataka maafisa manunuzi wa umma nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uzalendo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ufanisi na kuleta tija kwa taifa. Dk. Malik aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Pili wa mwaka wa maafisa Ununuzi wa Umma Zanzibar katika ukumbi wa Jaji mstaafu Hamid Mahmoud Hamid (ZEC) Maisara Alisema maafisa manunuzi ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa shughuli za serikali kutokana na nafasi yao katika kusimamia matumizi ya rasilimali za umma. Aidha alisema kada hiyo inapaswa kutambua wajibu wake wa msingi wa kusimamia sheria za manunuzi na kuhakikisha kila hatua ya mchakato wa ununuzi inafanyika kwa uwazi, uwajibikaji na kwa kuzingatia maslahi ya taifa. Alisisitiza kuwa maafisa hao wanapaswa kutanguliza uzalendo na maslahi ya nchi badala ya maslahi binafsi, huku wakitekeleza majukumu waliyopewa kwa mujibu wa sheria na mikataba ya ajira. Alisema serikali imekuwa ikipokea malalamiko kuhusu mikataba ambayo haitekelezwi ipasavyo au kushindwa kuilinda maslahi ya taifa hivyo aliwasisitiza  umuhimu wa kuandaa mikataba yenye tija na inayotekelezeka. Dk. Akil alisema sekta ya manunuzi ni mhimili mkubwa wa utekelezaji wa shughuli za serikali kwani takribani asilimia 80 ya shughuli za serikali zinategemea huduma za wataalamu wa manunuzi. Akizungumzia mageuzi ya mifumo, alisema serikali imeamua kuondokana na mifumo ya kienyeji kwa kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa e-Procurement System (ePROS) ili kuongeza uwazi, ufanisi na uwajibikaji katika manunuzi ya umma. Aliahidi kuwa serikali inaendelea kuithamini kada ya manunuzi kwa kuimarisha mfumo wa kisheria na mamlaka zinazosimamia sekta hiyo, huku mipango ikiendelea ya kuanzisha chombo cha kitaaluma kitakachosajili maafisa wote wa manunuzi nchini. Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza hadhi ya taaluma hiyo, kuimarisha uwajibikaji wa wataalamu na kuhakikisha maslahi yao yanazingatiwa sambamba na wajibu mkubwa walio nao katika kulinda rasilimali za taifa. Alisema ni imani yake mkutano huo utazaa matunda kwa kada hiyo ili kuona Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dk.Hamad Omar Fakih, alisema dhamira kubwa ya serikali ni kuhakikisha manunuzi ya umma yanafanyika kwa uwazi na weledi kwani taasisi hiyo ni muhimu kwa serikali. Aliwataka kutanguliza maslahi ya taifa ili kuhakikisha maendeleo ya nchi yaliyokusudiwa yanafikiwa. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Mohammed Fakih Mzee, alisema maofisa hao wana nafasi ya kipekee kuhakikisha fedha ya umma inatumika na inaleta matokeo yaliyousudiwa. Mapema Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa sera za Ununuzi wa Umma Zanzibar, Omar Said Omar, alisema mkutano huo umelenga kuimarisha uwazi wa ununuzi wa umma kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Alisema ununuzi wa umma ni nyenzo muhimu na kichocheo cha kimkakati kwa maendeleo ya Zanzibar na kukua kwa uchumi. Alibainusha kuwa lengo kuu ni kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati thabit katika utekelezaji  wa majukumu ya kila siku. Alisema malengo mengine ni kuimarisha mifumo ya kielektoriniki na kushirikisha sekta binafsi. Katika mkutano huo mada mbalimbali ziliwasilishwa ni pamoja na madhara ya rushwa kwa watumishi wa umma, changamoto ya mfumo wa kielktoriki wa katika ununuzi wa umma,

Uncategorized

UFUNGUZI WA MASJALA YA ARDHI

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuimarisha sekta ya ardhi kwa kujenga masjala za kisasa zitakazowezesha uhifadhi  kumbukumbu na taarifa za ardhi kwa mfumo wa kidijitali, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa huduma na kupunguza migogoro ya ardhi. Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akili, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hamad Bakar, wakati wa uzinduzi wa Masjala ya Ardhi Makunduchi, alisema Serikali imeamua kwa makusudi kuwekeza katika ujenzi wa masjala hizo ili kuimarisha usimamizi wa taarifa za ardhi nchini. Alisema mfumo huo wa kidijitali utawapa wananchi uhakika wa umiliki wa ardhi zao na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Aidha, aliitaka Kamisheni ya Ardhi kuhakikisha inakitumia kituo hicho kama kilivyokusudiwa ili kuimarisha mipango bora, imara na endelevu ya usimamizi wa ardhi. Aliongeza kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Tume ya Mipango inaendelea na ujenzi wa masjala nyingine katika Wilaya ya Chake Chake, Pemba, katika Kijiji cha Pujini. Amesema uhifadhi wa taarifa na nyaraka za ardhi ni muhimu katika kuzuia upotevu wa kumbukumbu na kupunguza migogoro ya ardhi isiyo ya lazima. Amefahamisha kuwa kupitia   mfumo huo utasaidia kuondoa dhuluma zinazoweza kujitokeza katika umiliki wa viwanja, kuiwezesha Serikali kuwa na kumbukumbu sahihi za ardhi, pamoja na kurahisisha shughuli za uhamishaji wa umiliki na utoaji wa hati kwa wananchi na wawekezaji. Akitoa taarifa ya kitaalamu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Dk. Afua Mohamed, amesema, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi inaendelea kutekeleza sera na mipango mbalimbali inayolenga kuimarisha usimamizi wa ardhi na kuimarisha utoaji wa huduma. Amesema Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi imekuwa ikiandaa mipango mbalimbali ya kuimarisha usimamizi wa ardhi nchini. Hata hivyo, alibainisha kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana, sekta ya ardhi bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo upotevu wa nyaraka muhimu za ardhi. Amesema Dhamira ya Serikali ya kujenga kituo hiki ni kuimarisha mifumo ya utunzaji wa taarifa na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa ardhi Ameleza kuwa ogezeko la mahitaji ya ardhi mwaka hadi mwaka linaifanya miundombinu hiyo kuwa muhimu, kwani kutokuwepo kwake kungeendelea kusababisha migogoro mingi ya ardhi. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhaza Gharib Juma, alisema masjala hiyo itakuwa hazina muhimu ya taarifa za ardhi ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikikabiliwa na changamoto za uhifadhi. Amesema vituo hivyo vina umuhimu mkubwa kwa kuwa vitatunza taarifa nyeti za taifa, hivyo akaomba viwekwe uzio kwa ajili ya kuimarisha usalama wake. Aidha, alisisitiza kuwa kutotambuliwa kwa ardhi kwa usahihi ndiko kunakochangia kuongezeka kwa migogoro mbalimbali, hususan ya mipaka. Ujenzi wa Masjala ya Ardhi Makunduchi umegharimu jumla ya shilingi milioni 560 hadi kukamilika kwake.

Uncategorized

NYENZO YA BAJETI YAZINDULIWA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imesema kwa kutambua umuhimu wa jinsia na wazee katika maendeleo ya kijamii kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imetenga bilioni 449 katika kutekeleza mpango huo.  Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Juma Malik Akil aliyasema hayo wakati akizindua nyenzo za bajeti inayozingatia jinsia (GRV) katika ukumbi wa Wazee Sebleni. Alisema hicho ni kiwango kikubwa ambacho kitawezesha kutekeleza jambo hilo kwa ufanisi kwani bajeti ya mwaka 2025/2026 ilitenga shilingi bilioni 70 pekee. Alifahamisha kuwa uzinduzi huo una umuhimu wa kipekee kwani unafanyika wakati Zanzibar inahitimisha utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) wa miaka mitano, 2021–2026. “Uzinduzi huu ni miongoni mwa mafanikio muhimu ya utekelezaji wa ahadi hizo na unaonesha dhamira ya serikali ya kuimarisha usawa wa kijinsia na uwajibikaji wa matumizi ya rasilimali za umma,” alisema. Alisema bajeti ndio nyenzo kuu ya serikali katika kutekeleza sera na mipango ya maendeleo kwani kupitia bajeti, serikali huamua namna rasilimali zitakavyogawiwa na huduma zitakavyotolewa kwa wananchi. Aidha alisema ni muhimu kuhakikisha kuwa maamuzi hayo yanazingatia mahitaji halisi ya wanawake, wanaume, wavulana  na wasichana ili kuwa na maendeleo jumuishi na yenye manufaa kwa wote. Dk. Malik alisema nyenzo hizo zitachangia utekelezaji wa Dira ya Zanzibar 2050, Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (ZADEP), Sera ya Jinsia ya Zanzibar ya mwaka 20216 na Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili wa mwaka 2025/2026– 2030. Waziri Malik alisisitiza kuwa uzinduzi wa vifaa hivyo si mwisho wa safari, bali ni mwanzo wa hatua mpya ya utekelezaji hivyo alizihimiza wizara, Idara na taasisi za serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Baraza la Wawakilishi, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatumika kikamilifu katika majukumu yao ya kila siku Alisema sasa kuna wizara tisa ambazo zinatekeleza mpango huo kwa majaribio na anaamini zitaweza kuongezeka ili kufikia katika kutekelekeza ngazi yote ya kitaifa. Aliipongeza UN Women kwa kuendelea kuwa mshirika muhimu wa serikali katika kuimarisha usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na kuendeleza utawala bora na maendeleo jumuishi, Umoja wa Ulaya (European Union) na Gates Foundation kwa msaada wao wa kifedha uliowezesha maandalizi, mapitio na ukamilishaji wa vifaa hivyo muhimu. Naye, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Anna Attanas Poul, alisema uzinduzi huo ni hatua muhimu kwani itaimarisha uwezo wa wizara na wadau wake kuhakikisha kuwa masuala ya kijinsia yanazingatiwa kikamilifu katika mipango, bajeti na utekelezaji wa programu za maendeleo. Alisema alisema UN Women kwa kushirikiana na washirika wake wameendelea kuiunga mkono serikali katika kuimarisha Bajeti Inayozingatia Jinsia na usimamizi wa fedha za umma unaozingatia usawa na ujumuishi. Kwa upande wake Mwakilishi wa UN Women Tanzania, Catharine Gifford, alisema bajeti inayozingatia jinsia ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha rasilimali za umma zinawanufaisha wananchi wote kwa usawa bila kujali jinsia. Aliipongeza SMZ kwa juhudi zake za kuingiza masuala ya kijinsia katika mifumo ya mipango na bajeti kwani bajeti inayozingatia jinsia sio bajeti maalumu kwa wanawake au wanaume pekee bali ni mfumo unaolenga kuhakikisha sera, mipango na matumizi ya fedha za umma yanazingatia mahitaji ya wanawake, wanaume, wasichana na wavulana kwa usawa. Alibainisha kuwa mbinu hiyo husaidia kubaini makundi yanayonufaika na matumizi ya umma na yale yanayoweza kubaki nyuma katika mchakato wa maendeleo. Hivyo, aliahidi kuwa UN Women itaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali ili kuhakikisha masuala ya kijinsia yanaingizwa kikamilifu katika upangaji wa mipango, ugawaji wa bajeti na utoaji wa huduma kwa wananchi wote.

Uncategorized

BAJETI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KUWASILISWA

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil, amebainisha vipaumbele tisa vya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/2027, vikiwemo kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kusimamia utekelezaji wa bajeti inayozingatia usawa wa kijinsia pamoja na kupitia sera, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kurahisisha utoaji wa huduma za Serikali. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katika kikao cha 30 cha Baraza la Wawakilishi kilichofanyika Chukwani, Dkt. Juma amesema wizara hiyo itaendelea kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kuweka mazingira bora yatakayochochea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar. Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya bajeti ya Baraza la Wawakilishi, Bakari Hamad Bakar, amesema kamati hiyo inashauri wizara kuhakikisha kunakuwepo na matumizi yenye tija ya fedha za umma ili mipango iliyopangwa iweze kutekelezwa kwa ufanisi na kuleta manufaa kwa wananchi pamoja na kukuza uchumi wa nchi. Wakati huo huo, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia hotuba hiyo wamesisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuongeza uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Akijibu hoja za wajumbe, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil, amesema Serikali itaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo yote yenye lengo la kuimarisha usimamizi wa fedha za umma, kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa bajeti na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Zanzibar. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliipitisha bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya zaidi ya shilingi trilioni nane kwa ajili ya kutekelezav majukumu na vipaumbele vilivyoainishwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Uncategorized

MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KOREA

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndugu Aboud Hasan Mwinyi ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Makatibu Wakuu wa nchi za Afrika na Korea uliofanyika jijini Seoul nchini Korea. Mkutano huo umefanyika tarehe 1 na 2 Juni, 2026.

Scroll to Top